• HABARI MPYA

    Wednesday, January 04, 2017

    FARID SASA ANGOJA LESENI TU YA RFEF AANZE KAZI SEGUNDA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WINGA chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Farid Malik Mussa amesema kwamba anasubiri leseni ya Mamlaka ya Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) aanze kuchezea klabu yake, Club Deportivo Tenerife.
    Farid amejiunga na klabu hiyo ya Santa Cruz de Tenerife, Tenerife, visiwa vya Canary mwezi huu kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.
    Na tangu afike wiki iliyopita amekuwa akifanya mazoezi tu na timu hiyo ya Daraja la Kwanza, maarufu kama Segunda Division, inayotumia Uwanja wa Heliodoro Rodriguez Lopez wenye kuchukua mashabiki 23,660.
    Farid Mussa Malik akiwa na vifaa vya michezo alivyopatiwa baada ya kuwasili Tenerife
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online kwa simu jana usiku, Farid alisema anaendelea vizuri tangu afike na amekuwa akifanya mazoezi na wenzake, lakini hajaanza kicheza Ligi kwa sababu ya leseni.
    “Nadhani leseni itatoka wakati wowote. Sitarajii kama itachelewa,”alisema Farid.
    Azam FC imemtoa kwa mkopo Farid kwenda CD Tenerife kwa makubaliano maalum baada ya winga huyo kufuzu majaribio katika klabu hiyo Aprili mwaka jana alipokwenda na Mkurugenzi wa klabu yake, Yussuf Bakhresa.
    Farid alitua Hispania Aprili 21 baada ya kuichezea Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance mjini Tunis, Tunisia ikifungwa 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam.
    Na ilimchukua wiki moja tu Farid kuwakuna kwa kipaji chake makocha wa Tenerife na kutaka kumnunua, lakini Azam ikakataa na kuamua kumtoa kwa mkopo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FARID SASA ANGOJA LESENI TU YA RFEF AANZE KAZI SEGUNDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top