• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 24, 2017

  PIGO SIMBA SC, KAHEMELE ANG'ATUKA NA KUREJEA AZAM

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM 
  KATIBU wa Simba, Patrick Kahemele ameachia ngazi na kuerejea kampuni ya Bakhresa Group Limited.  
  Kahemele aliyekuwa Katibu wa Simba tangu Juni mwaka jana, anarejea Bakhresa Group kwenda kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Michezo ya Azam TV, nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Charles Hilary.
  Gwiji wa Habari, Charles Hillary sasa anakwenda kuwa Mkurugenzi Utayarishaji wa Vipindi vya Televisheni vya Azam TV.   
  Patrick Kahemele (kushoto) ameachia ngazi na kuerejea kampuni ya Bakhresa Group Limited 

  Katika kipindi chake kifupi cha kufanya kazi Simba, Kahemele alionyesha dira ya mabadiliko kabla ya kuondoka ghafla na kurejea Azam.
  Wazi kuondoka kwa Kahemele aliyeibukia Mtibwa Sugar na baadaye akawa Meneja wa Azam FC na mwasisi wa Azam TV ni pengo kwa Simba. 
  Bila shaka, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collin Frisch atarejea kukaimu nafasi hiyo wakjati klabu inatafuta mtu mwingine.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PIGO SIMBA SC, KAHEMELE ANG'ATUKA NA KUREJEA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top