• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 28, 2017

  PATASHIKA LEO AFCON SENEGAL NA CAMEROON

  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limesema kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya viwanja kwa mechi za Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mjini Franceville na Libreville.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari, Ofisa Habari wa (CAF), Junior Binyam alipuuza malalamiko yote ya makocha juu ya ugumu wa maeneo ya kuchezea kwenye viwanja hivyo.
  “Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba ugumu wa maeneo ya kuchezea ya viwanja ndiyo unasababisha wachezaji kuumia. Viwanja havijatumika kwa siku nne, hivyo watapona,” alisema Binyam.
  Mshambuliaji tegemeo wa Senegal, Sadio Mane ataiongoza timu yake dhidi ya Cameroon leo

  Taarifa za vyombo vya Habari zinasema kwamba viwanja mjini Port Gentil na Oyem havistahili kwa mechi za Robo Fainali kutokana na ugumu wake kwenye maeneo ya kuchezea.
  Uwanja wa d’Oyem ulimwagiwa maji wakati wa mechi kati ya Uganda na Mali Jumatano ili kuulainisha, wakati Uwanja wa Port Gentil umelalamikiwa na timu zote za Kundi D zikiwemo Misri, Ghana, Mali na Uganda.
  Leo Burkina Faso itamenyana na Tunisia mjini Libreville wakati Senegal itaumana na Cameroon mjini Franceville katika Robo Fainali. Misri na Morocco zitamenyana kesho mjini Libreville wakati Ghana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zitahitimisha mechi za Robo Fainali kwa kumenyana mjini Port Gentil kesho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PATASHIKA LEO AFCON SENEGAL NA CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top