• HABARI MPYA

    Thursday, January 26, 2017

    MICHO AJIVUNIA KIWANGO CHA UGANDA

    KOCHA wa Uganda, Milutin ‘Micho’ Sredojevic amesema kwamba amevutiwa na kiwango cha timu yake licha ya kuambulia pointi moja katika Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017 nchini Gabon na kutolewa hatua ya makundi.
    Mtaalamu huyo wa Kiserbia, ambaye ameirejesha The Cranes kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978, alisema ameshuhudia kiwango cha timu yake kikipanda kwa kiasi kikubwa katika siku 11 zilizopita.
    Micho amesema amevutiwa na kiwango cha Uganda yake licha ya kuambulia pointi moja AFCON 

    “Najivunia wachezaji na walichovuna kwenye mashindano haya. Hatukuwa timu nyepesi mbele ya timu kubwa kama Misri, Ghana na Mali ambazo zina wachezaji wazoefu sana, lakini tumeonyesha kwamba tunaweza kushindana katika hiki,” alisema Micho.
    Uganda ilifungwa 1-0 kwa bao la penalti dakika ya 30 dhidi ya Ghana katika mchezo wao wa ufunguzi Januari 17 kabla ya kuchapwa 1-0  na mabingwa mara saba, Misri kwa bao la dakika ya 88 la El Said Jumamosi iliyopita mjini Port Gentil.
    Katika mchezo wa juzi dhidi ya Mali, nyota kijana mdogo, Farouk Miya alitangulia kuifungia Cranes dakika ya 69 kabla ya mchezaji tegemeo wa Mali kwa sasa, Yves Bissouma kuisawazishia timu yake dakika tatu baadaye.
    Micho anashiwishika kuamini kwamba licha ya timu yake kutolewa mapema, lakini ilionyesha kiwango kizuri ikishiri AFCON baada ya miaka 39 iiposhiriki mara ya mwisho.
    Uganda ilishika mkia katika Kundi D kwa pointi yake moja na inarejea nyumbani kujipanga mwa mechi za kufuzu AFCON ya 2019, Kombe la Dunia la FIFA nw mechi za kufuzu Chan 2018.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHO AJIVUNIA KIWANGO CHA UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top