• HABARI MPYA

    Tuesday, January 24, 2017

    YANGA WAOMBA MECHI ZAO ZOTE ZIPIGWE TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Yanga jana imeandika barua Wizara ya Habari Sanaa na Utamaduni na Michezo kuomba iruhusiwe kuanzia wikiendi hii kutumia Uwanja wa Taifa, badala ya Uhuru mjini Dar es Salaam kwa mechi zake za mashindano ya nyumbani.
    Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit aliiambia Bin Zubeiry Sports - Online jana mjini Dar es Salaam kwamba ombi linatokana na kwamba wamekaribia kuingia kwenye michuano ya Afrika, ambayo watatumia Uwanja wa Taifa.
    Kwa sababu hiyo, Baraka alisema wanataka waruhusiwe kuanza kuutumia Uwanja wa Taifa, ili wauzoeee mapema hata mechi zao za michuano ya Afrka itakapoanza wawe tayari.
    Kaimu Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit (katikati) akiwa na rafiki zake

    “Kama unavyojua kwa muda mrefu hatujautumia Uwanja wa wetu huu kipenzi wa Taifa baada ya kuzuiwa na Serikali kufuatia vurugu za kwenye mechi yetu na Simba baada ya mashabiki wa wenzetu kufanya fujo na kuvunja viti,”.
    “Lakini pia kama utakumbuka baadaye sisi (Yanga) tuliingia mkataba maalum na Serikali wa kuutumia Uwanja huu kwa mechi za mashindano ya Afrika na ule wa Uhuru kwa Ligi Kuu pekee. Hivyo kwa kuwa tunakaribia kuanza mechi za Afrika, tunaiomba Serikali ituruhusu kuhamishia mechi zetu za mashindano ya nyumbani Uwanja wa Taifa, ili iwe sehemu ya maandalizi yetu ya michuano hiyo ya Afrika,”alisema Baraka.
    Yanga SC watakuwa wenyeji wa Mwadui FC ya Shinyanga Januari 29 mjini Dar es Salaam na baada ya hapo, itaikaribisha Stand United Februari 5, mwaka huu kabla ya kuingia kwenye michuano ya Afrika.
    Februari 10, mwaka huu, Yanga watakuwa wageni wa Ngaya FC katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mde mjini Mde nchini Comoro, kabla ya kurudiana Februari 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAOMBA MECHI ZAO ZOTE ZIPIGWE TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top