• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 29, 2017

  WENGER AFUNGIWA MECHI NNE ENGLAND

  KOCHA Arsene Wenger amefungiwa mechi nne na Chama cha Soka England baada ya tukio alilolifanya wakiifunga Burnley.
  Wenger alianza kutumikia adhabu hyake jana akikosa mchezo wa Kombe la FA ambao kwa bahati nzuri timu yake ilishinda 5-0 dhidi ya wenyeji Southampton, lakini atakosa mechi dhidi ya Watford, vinara Chelsea na Hull City.
  Wenger aliodolewa uwanjani na refa Jon Moss baada ya kudaiwa kumtolea maneno machafu refa wa akiba, Anthony Taylor kufuatia Burnley kupewa penalrti dakika ya mwisho Uwanja wa Emirates.
  Kocha huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 67, ambaye Arsenal yake ilishinda 2-1 siku hiyo, pia ametozwa faini ya Pauni 25000 baada ya kukiri makosa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WENGER AFUNGIWA MECHI NNE ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top