• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 27, 2017

  NI BARCELONA NA ATLETICO MADRID NUSU FAINALI KOMBE LA MFALME

  TIMU za Atletico Madrid na Barcelona zitamenyana na katika Nusu Fainali za Kombe la Mfalme kuanzia Ijumaa.
  Celta Vigo itamenyana na Alaves katika Nusu Fainali nyingine za nyumbani na ugenini Februari 1 na 8.
  Mchezo wa mwisho kuzikutanisha timu hizo Atletico Madrid walishinda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (1-2 na 2-0) Aprili mwaka jana.
  Mara ya mwisho zilipokutana kwenye Kombe la Mfalme, Barcelona ilishinda (1-0 na 3-2) na wakaenda kubeba taji hilo mwaka 2015, ambao ulikuwa wa mafanikio makubwa kwao.
  Lionel Messi (kulia) akiichezea Barcelona jana dhidi ya Real Sociedad  

  Atletico walikuwa mabingwa wa La Liga, lakini wakafungwa mechi ya kwanza ya Nusu Fainali mwaka 2015 mjini Katalunya kabla ya mchezo mkali wa marudiano ambao zilitoka kadi 11 za njano na nyekundu moja kabla ya Neymar kufunga mabao mawili, Barcelona ikishinda 3-2 usiku huo.
  Mabao mawili ya Antoine Griezman katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa yaliipa Atletico ushindi mwaka 2015.
  Katikati ya wiki Barcelona ilishinda kwa jumla ya mabao 6-2 kwenye Robo Fainali wakiitoa Real Sociedad wakati Atletico iliifunga Eibar 5-2.
  Maajabu zaidi katika Robo Fainali yalikuwa ni kutolewa kwa Real Madrid kwa jumla ya mabao 4-3 wakifungwa na Celta Vigo, wakati Alavas iliifunga timu ya Daraja la Pili, Alcorcon.
  Mechi za kwanza za Nusu zitachezwa Februari 1 na 2 na marudiano Februari 8.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI BARCELONA NA ATLETICO MADRID NUSU FAINALI KOMBE LA MFALME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top