• HABARI MPYA

    Monday, January 30, 2017

    MALARIA YAMKWAMISHA BOSSOU TOGO

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka la Togo (FTF) limeiandikia barua klabu ya Yanga kumuombea ruhusa beki Vincent Bossou kwamba atachelewa kurejea kwa sababu anasumbuliwa na Malaria.
    Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba wamepokea barua kutoka FTF ikimuombea ruhusa Bossou.
    “Sasa tunamtarajia kufika hapa kuanzia Jumatano baada ya kupokea barua ya FTF kwamba alipatwa Malaria, hivyo hakuweza kuondoka mapema kama ilivyotarajiwa,”alisema. 
    Bossou alikuwa nchini Gabon kwenye AFCON, ambako kwa bahati mbaya timu yake, Togo imetolewa baada ya hatua ya makundi tu kufuatia kuambulia pointi moja tu baada ya mechi za tatu za Kundi A.
    FTF imeiandikia barua Yanga kumuombea ruhusa Vincent Bossou atachelewa kurejea kwa sababu anasumbuliwa na Malaria

    Ilifungwa 3-1 mara mbili na Morocco na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kutoa sare ya 0-0 na Ivory Coast na kwa bahati mbaya mechi zote hizo Bossou alikuwa benchi hakucheza.  
    Wachezaji wengine wa Ligi Kuu ya Bara waliokuwa AFCON ni beki wa Simba, Juuko Murshid aliyekuwa na kikosi cha Uganda na winga Bruce Kangwa wa Azam FC aliyekuwa na Zimbabwe, ambao wote timu zao hazikuvuta hatua ya makundi.
    Zimbawe walishika mkia Kundi C wakiambulia pointi moja baada ya kufungwa mechi mbili na sare moja, sawa na Uganda walioshika mkia Kundi D pia kwa kuambulia pointi moja baada ya sare moja na kufungwa mechi mbili. 
    Wakati huo huo; Baraka amesema mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma anatarajiwa kurejea kesho Dar ea Salaam baada ya kukosekana kwa takriban wiki tatu.
    Ngoma aliyekwenda kwao, Zimbabwe kwa matatizo ya kifamilia, alionfoka nchini akiwa majeruhi baada ya kuumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALARIA YAMKWAMISHA BOSSOU TOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top