• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 30, 2017

  MISRI WATINGA NUSU FAINALI AFCON, WAILAZA 1-0 MOROCCO

  BAO la dakika ya 87 la Mahmoud Kahraba jana limetosha kuipeleka Nusu Fainali Misri baada ya kuilaza 1-0 katika Robo Fainali ya mwisho ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mjini Port-Gentil, Gabon.
  Kahraba alifunga bao hilo baada ya kukutana na mpira uliomgonga Ahmed Hassan kufuatia kona na kuusukumia nyavuni kiulaini na kuzima ndoto za kocha wa Morocco, Mfaransa Herve Renard kutwaa taji la tatu la AFCON.
  Mfungaji wa bao pekee la Misri, Mahmoud Kahraba (katikati) akipongezwa na wenzake PICHA ZAIDI GONGA HAPA  
  Ushindi huo wa kwanza kwa Mafarao wa Misri dhidi ya wapinzani wao hao wa Kaskazini mwa Afrika baada ya zaidi ya miaka 30 unawafanya wakutane na Burkina Faso kwenye Nusu Fainali Jumatano, wakati Ghana itamenyana na Cameroon.
  Kikosi cha Misri jana kilikuwa; El Hadary; Elmohamady, Gabr, Hegazy, Fathy; Hamed, Hafez/Kahraba dk62, Salah, El Said, M Hassan, Mohsen/A Hassan dk43, El Said na Kahraba.
  Morocco; Mohand; Da Costa, Benatia, Saiss/Alioui dk92, Dirar, El Ahmadi, Boussoufa, Mendyl, Fajr, En-Nesyri na Bouhaddouz/El Kaddouri dk78.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MISRI WATINGA NUSU FAINALI AFCON, WAILAZA 1-0 MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top