• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 31, 2017

  CHIRWA: SHUGHULI NDIYO IMEANZA SASA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Mzambia wa Yanga, Obrey Chirwa amesema kwamba mabao aliyofunga juzi dhidi ya Mwadui FC ni kama yamemzindua upya na sasa mashabiki wa timu hiyo watarajie makubwa kutoka kwake.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online jana, Chirwa alisema kwamba amefurahi kufunga mabao hayo, kwani ameiwezesha timu yake kurejea juu ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya muda mrefu.
  “Nina furaha sana, nimefunga mabao muhimu na tumeshinda mchezo huu uliokuwa mgumu na tumefanikiwa kuongoza tena Ligi Kuu,”alisema Chirwa.
  Obrey Chirwa amesemamabao aliyofunga juzi dhidi ya Mwadui FC ni kama yamemzindua upya  

  Mzambia huyo, jana alitokea benchi na kufunga mabao yote, Yanga ikiilaza 2-0 Mwadui FC ya Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaipandisha Yanga SC kileleni mwa Ligi Kuu ikifikisha pointi 46 baada ya kucheza mechi 20, ikiwashushia nafasi ya pili Simba SC waliojinafasi  kileleni kwa muda mrefu tangu kuanza kwa ligi hiyo Septemba mwaka jana.
  Chirwa alifunga mabao yote hayo kipindi cha pili baada ya kuingia kuchukua nafasi ya kiungo wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima kipindi cha pili.
  Chirwa aliyesajiliwa msimu huu kutoka FC Platinums ya Zimbabwe, alifunga bao la kwanza dakika ya 69 kwa shuti kali akiuwahi mpira uliookolewa na kipa wa Mwadui FC, Shaaban Hassan Kado baada ya shuti la Simon Msuva na la pili dakika ya 82 kwa shuti baada ya kudondoshewa pasi ya kichwa na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko kufuatia krosi ya beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHIRWA: SHUGHULI NDIYO IMEANZA SASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top