• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 31, 2017

  WACHEZAJI CAMEROON WAGOMEA MAZOEZI SABABU YA POSHO

  WACHEZAJI wa Cameroon jana waligoma kufanya mazoezi nchini Gabon kwa sababu ya posho.
  Simba Wasiofungika wanadai posho zao baada ya kuiwezesha timu kufika Nusu Fainali, wakiitoa timu ngumu Senegal kwa penalti 5-4 katika Robo Fainali.
  Taarifa kutoka kwenye kambi ya timu hiyo imesema kwamba vijana wa Hugo Broos wanadai CFA faranga Milioni 12 kwa ajili ya Robo Fainali na Nusu Fainali.
  Serikali iliwaahidi wachezaji hao CFA faranga Milioni 10 kila mchezaji baada ya awali kukataa pendekezo la CFA faranga Milioni 4.
  Nahodha Benjamin Moukandjo na wachezaji wenzake walikataa fedha hizo hadi wakapandishiwa dau. Wachezaji wameomba kukutana na Serikali ili walipwe fedha zao kamili kabla hawajaingia kucheza na Ghana Alhamisi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WACHEZAJI CAMEROON WAGOMEA MAZOEZI SABABU YA POSHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top