• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 27, 2017

  ASAMOAH GYAN FITI KUWAVAA DRC JUMAPILI

  TIMU ya taifa ya Ghana inatarajia nahodha na mshambuliaji wake tegemeo, Asamoah Gyan atakuwa tayari kucheza Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya kufanyiwa vipimo vya maumivu aliyoyapata Jumatani.
  Taaifa ya FA ya Ghana imesema mshambuliaji huyo amerejea  kwenye kambi ya timu mjini Oyem, Kaskani mwa Gabon kuendelea na matibabu ya shingo aliyoyapata wakifungwa 1-0 na Misri katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi D mjini Port-Gentil.
  Asamoah Gyan atakuwa tayari kucheza Robo Fainali ya AFCON dhidi ya DRC Jumapili

  "Vipimo alivyofanyiwa katika mji mkuu wa Gabon, Libreville vimeonyesha maumivu si makubwa kama ilivyohofiwa baada ya kuumia,"imesema taarifa hiyo.
  "Gyan sasa amejiunga na kambi ya Black Stars mjini Oyem kuendelea na matibabu ya kumfanya awe fiti kikamilifu,".
  Gyan, mshambuliaji wa zamani wa Udinese ya Italia, Rennes ya Ufaransa na Sunderland ya England, hadi sasa ameichezea mechi 99 Ghana na kufunga mabao 49.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ASAMOAH GYAN FITI KUWAVAA DRC JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top