• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 24, 2017

  JKT RUVU SASA UWANJA WA NYUMBANI MKWAKWANI, TANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeridhia ombi la klabu ya JKT Ruvu kuhamia Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kutoka Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  TFF imekubali ombi hilo baada ya kuzingatia hoja ya JKT Ruvu Stars kwamba wachezaji wake 12 wa kikosi cha kwanza wamekwenda kwenye mafunzo ya kijeshi mkoani Tanga.
  "Ombi hilo limekubaliwa. Kwa mujibu wa Kanuni ya 6(6) ya Ligi Kuu, TFF/TPLB zina mamlaka ya mwisho kuhamisha kituo cha mchezo kwa sababu inazoona zinafaa na kwa wakati husika,".
  Aidha, malalamiko ya klabu za Mwadui FC na Polisi Morogoro kuhusu uhalali wa usajili wa mchezaji wa Stand United, Kheri Mohamed Khalifa na wachezaji wawili wa Njombe Mji kucheza mechi bila leseni yamepelekwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.
  Pia maombi ya klabu ya Singida United kuhusu kubadilishiwa Mwamuzi kwenye mechi yao yamepelekwa Kamati ya Waamuzi, wakati maombi ya Alliance Schools, Friends Rangers FC, The Mighty Elephant na Kariakoo FC yanayohusu uendeshaji yanashughulikiwa na Sekretarieti ya TPLB.
  Pia Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF inatarajiwa kukaa wiki ijayo kusikiliza malalamiko dhidi ya usajili wa wachezaji mbalimbali akiwemo mchezaji Venance Joseph Ludovic.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JKT RUVU SASA UWANJA WA NYUMBANI MKWAKWANI, TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top