• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 29, 2017

  WATOTO WA PELE WAIPELEKA GHANA NUSU FAINALI AFCON

  NDUGU Andre na Jordan Ayew wamefunga mabao kuiwezesha Ghana kuingia Nusu Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa d'Oyem nchini Gabon leo.
  Watoto hao wa Mwanasoka Bora wa zamani Afrika, Abedi Ayew 'Pele' na gwiji wa Ghana, walifunga mabao yao kipindi cha pili katika mchezo mgumu wa Robo Fainali leo.
  Jordan alianza kufunga bao zuri dakika ya 63 akimpndua beki wa DRC baada ya pasi ya Mubarak Wakaso na kufumua shuti zuri lililompita kipa hodari, Vumi Ley Matampi.
  Lakini Paul-Jose M'Poku akaisawazishia DRC dakika ya 68 kwa shuti la mbali baada ya pasi ya Chancel Mbemba Mangulu, kabla ya Nahodha, Andre Ayew kufunga la ushindi kwa penalti dakika ya 78.
  Nahodha wa Ghana, Andrew Ayew (katikati) akikimbia na webzake kushangilia baada ya kufunga bvao la ushindi PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Ghana inaungana na Burkina Faso na Cameroon kwenda Nusu Fainali, wakati mchezo kati ya Misri na Morocco unaofuatia leo usiku utakamilisha idadi ya timu nne za Nusu Fainali.
  Kikosi cha Ghana kilikuwa; Razak, Acheampong, Boye, Amartey, Afful, Wakaso, Acquah, Partey, Atsu, A. Ayew na J.Ayew.
  DRC: Matampi; Lomalisa, Tisserand, Bope, Mpeko - Kabananga, Mbemba, Mulumba/Bolingi dk85, Mubele/Bokila dk83, M'Poku/Bakambu dk83 na Mbokani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WATOTO WA PELE WAIPELEKA GHANA NUSU FAINALI AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top