• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 29, 2017

  BOCCO AFICHUA SIRI YA KUWAFUNGA SIMBA SC

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ amesema kwamba utulivu na kutokata tamaa ndiyo imekuwa siri ya mafanikio yake kuifunga mara nyingi Simba SC. 
  Bocco alifunga bao pekee dakika ya 70 jana Azam FC ikiilaza Simba SC 1-0 katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Na baada ya mchezo huok Bocco alisema kwamba kufunga kwake kwenye mechi nyingi dhidi ya Simba kutokana na utulivu na kutokata tamaa muda wote wa mchezo.
  John Bocco ‘Adebayor’ amesema kwamba utulivu na kutokata tamaa ndiyo sababu ya kuifunga mara nyingi Simba SC 

  “Kila mechi nawekewa ulinzi mkali, lakini sikati tamaa, muda wote ninakuwa na lengo moja tu la kutafuta nafasi ya kufunga, ambalo ndilo jukumu langu nililopewa uwanjani kama mshambuliaji,”alisema Bocco na kuongeza.
  “Mfano mechi kama ya leo (juzi) mimi ninapenda niwasifu mabeki wa Simba walicheza vizuri na kutubana kwa muda mrefu, lakini likatokea kosa moja tu na sisi tukalitumia vizuri kujipatia bao,”alisema Bocco.   
  Bao la juzi linakuwa la nane kwa Bocco msimu huu na sasa anazidiwa kwa bao moja na Amissi Tambwe, Simon Msuva wa Yanga na Shiza Kichuya wa Simba wanaoongoza kwa pamoja kila mmoja akiwa na mabao tisa.
  Aidha, juzi Bocco aliifikisha mabao 19 ya kuifunga Simba tangu Azam ipande Ligi Kuu mwaka 2008, hivyo kuendelea kuongoza kufunga mabao mengi katika mechi baina ya timu hizo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BOCCO AFICHUA SIRI YA KUWAFUNGA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top