• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 26, 2017

  UGANDA WAAMBULIA POINTI MOJA AFCON

  ANGALAU wanarudi na kusimulia nyumbani. Uganda imeambulia pointi moja na bao moja katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu nchini Gabon baada ya sare ya 1-1 na Mali katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Jumatano.
  Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa d'Oyem uliokuwa vidimbwi vya maji baada ya mvua kunyesha, Faruku Miya alitangulia kuwafungia Uganda dakika ya 69 kabla ua Yves Bissouma kuwasawazishia Mali dakika ya 73. 
  Mali inamaliza nafasi ya tatu katika Kundi D kwa pointi zake mbili za sare mbili na kufungwa mechi moja, wakati Uganda iliyopoteza mechi mbili kwavipigo vya 1-0 mara zote mbele ya Misri na Uganda kabla ya sare na Mali, inamaliza mkiani kwa pointi yake moja.
  Uganda iliyokuwa ikicheza AFCON ya kwanza baada ya miaka 39, inarejea nyumbani kwa pamoja na Mali, huku Ghana na Misri timu nyingine katika kundi hilo zikienda Robo Fainali.
  Kikosi cha Uganda kilikuwa: Odongkara, Ochaya, Kizito, Juuko, Iguma, Aucho/Azira dk90, L. Kizito/Massa dk79, Oloya/Mawejje dk59, Walusimbi, W. M. Hassan na Miya. 
  Mali: Sissoko, Hamari, Wague, O. Coulibaly, L. Coulibaly/K. Coulibaly dk53, Sylla, N'Diaye, Bissouma, M. N'Diaye, Marega/Yatabare dk80 na Doumbia.
  Wakati huo huo: Robo Fainali za AFCON zinatarajiwa kufanyika Jumamosi na Jumapili wiki hii.
  Jumamosi Burkina Faso wataanza na Tunisia Uwanja wa d'Angondje Saa 1:00 usiku, kabla ya Senegal kumenyana na Cameroon Uwanja wa Franceville Saa 4:00 usiku.
  Jumapili Jamhuri ya KIdemokrasia ya Kongo (DRC) itamenyana na Ghana wakati Uwanja wa d'Oyem Saa 1:00 usiku wakati Misri itavaana na Morocco Uwanja wa Port Gentil Saa 4:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UGANDA WAAMBULIA POINTI MOJA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top