• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 27, 2017

  SIMBA YAMTOA KWA MKOPO BLAGNON OMAN CLUB

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imemtoa kwa mkopo wa miezi sita mshambuliaji wake, Muivory Coast, Frederick Blagnon kwenda klabu ya Oman FC ya Oman.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara alisema jana katika mazungumzo na Bin Zubeiry Sports - Online jana kwamba, Blagnon wameamua kumtoa mkopo mchezaji huyo baada ya kutoridhishwa na dau la Oman Club kumununua moja kwa moja.
  “Oman Club hawakuwa na ofa nzuri sana kwa kuwauzia moja kwa moja mchezaji huyo, hivyo tumeona tuwape kwa mkopo kwanza, kama watavutiwa naye na kuongeza dau, tutawapa moja kwa moja,”alisema. 
  Frederick Blagnon (kushoto) akiwa kwenye benchi Simba SC

  Blagnon anakuwa mchezaji wa pili wa Simba kutolewa kwa mkopo Oman, baada ya mshambuliaji mwingine, mzalendo Daniel Lyanga kutolewa kwa mkopo pia Fanja ya Oman. 
  Na wawili hao wanafanya idadi ya jumla ya wachezaji wa Simba wanaocheza kwa mkopo kufika watano, baada ya wengine watatu kutolewa kwa mkopo kwenye timu mbalimbali za hapa nyumbani.
  Hao ni beki Emmanuel Semwanza aliyepelekwa Maji Maji ya Songea na viungo 
  Awadh Juma aliyepelekwa Mwadui FC ya Shinyanga na Peter Mwalyanzi aliyepelekwa African Lyon ya Dar es Salaam.
  Blagnon alijiunga na Simba SC kwa dau la Sh. Milioni 100 kutoka African Sports ya kwao, Ivory Cioats Julai mwaka jana, lakini pamoja na kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubw azaidi kikosini, akashindwa kuonyesha thamani yake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA YAMTOA KWA MKOPO BLAGNON OMAN CLUB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top