• HABARI MPYA

  Friday, January 27, 2017

  ONOKA KUCHEZESHA SIMBA NA AZAM KESHO, MWANAMKE KUWACHEZESHA YANGA JUMAPILI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  REFA Erick Onoka wa Arusha atachezesha mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho kati ya Simba SC na Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Onoka atasaidiwa na washika vibendera Hassan Zani wa Arusha na Josephat Masija wa Mwanza, wakati mezani atakuwapo Soud Lila wa Dar es Salaam na Kamisaa ni Michael Bundala wa Dar es Salaam.
  Timu hizo zitakutana tena kesho ikiwa ni kiasi cha wiki mbili tangu zimenyane kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi na bao pekee la Himid Mao kwa shuti la mbali likaipa Azam ushindi wa 1-0 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Kwa Azam ushindi huo ulikuwa sawa na kulipa kisasi cha kipigo kama hicho cha 1-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Septemba 17, mwaka jana Uwanja Uhuru, Dar es Salaam bao pekee la Shiza Kichuya.
  Mchezo wa Jumapili kati ya Yanga na Mwadui FC ya Shinyanga utachezeshwa na Jonesiya Rukyaa wa Kagera, atakayesaidiwa na washika vibendera Hassan Sika wa Pwani na Haji Mwalukuta wa Tanga, wakati mezani atakuwapo Omar Kambangwa wa Tanga na Kamisaa 
  Bili Mwilima wa Arusha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ONOKA KUCHEZESHA SIMBA NA AZAM KESHO, MWANAMKE KUWACHEZESHA YANGA JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top