• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 24, 2017

  LIGI YA WANAWAKE KUENDELEA KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI ya wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano Januari 25, mwaka huu kwa michezo sita – mitatu kwa kila kundi.
  Kundi A, linatarajiwa kuna na mchezo kati ya JKT Queens Dar es Salaam na Mburahati Queens pia ya jijini utakaofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala.
  Kadhalika Viva Queens ya Mtwara itakuwa mwenyeji wa Evergreen ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati Mlandizi ya mkoani Pwani itakuwa mgeni wa Fair Play katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
  Kwa upande Kundi B, Sisterz ya Kigoma itaikaribisha na Baobab ya Dodoma kwenye mfululizo wa ligi hiyo. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Lake Tanganyika.
  Mchezo mwingine utachezwa Uwanja wa Samora mkoani Iringa kati ya Panama na Majengo Women ya Singida ilihali Victoria Queens ya Kagera na Marsh Academy zitapambana hiyo kesho kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Kagera.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIGI YA WANAWAKE KUENDELEA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top