• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 27, 2017

  TFF YAMSHUKURU RAIS DK. MAGUFULI KUUFUNGULIA UWANJA WA TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli kwa kuridhia kufunguliwa tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kadhalika, TFF imeishukuru Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa juhudi zake na kwamba namna ilivyoonyesha ushirikiano kufanikisha suala la kufunguliwa uwanja huo uliofungiwa matumizi yake na Serikali, Oktoba mwaka uliopita.
  "TFF inachukua nafasi hii kuahidi kuwa itasimamia matumizi mazuri ya uwanja huo kwa kutoa elimu kwa wadau ili kuutumia uwanja huo vema ikitambua kuwa ni hazina ambayo imetokana na nguvu na gharama kubwa za Serikali kuujenga uwanja huo,"imesema taarifa ya TFF.
  Aisha, TFF imetahadharisha mashabiki wa mpira wa miguu kwamba uwanja huo umejengwa kwa gharama kubwa hivyo ni jukumu lao kuutuza na kuutumia vema kwa sababu ni hazina kubwa waliyonayo na ni miongoni mwa urithi bora kwa vizazi vijavyo.
  TFF imesema imetuma maombi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuomba kuutumia uwanja huo kwenye mchezo wa leo Jumamosi Januari 28, mwaka huu kati Simba na Azam na keshokutwa katika mchezo kati ya Yanga ya Dar es Salaam na Mwadui ya Shinyanga.
  Uwanja wa Taifa ulifungwa baada ya mechi ya Simba na Yanga Oktoba 1, mwaka jana bao la Amissi Tambwe ilikiwa chanzo

  Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inaonesha kuwa ligi hiyo huko Mbeya kutakuwa na ‘derby’ kwa maana ya mchezo wa upinzani baina ya timu zinazotoka mkoa mmoja wa Mbeya ambazo ni Tanzania Prisons na Mbeya City utakaochezwa na Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
  Keshokutwa Jumapili Januari 29, mwaka huu kutakuwa na mchezo mwingine ambao Yanga itacheza na Mwadui jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Majimaji ya Songea itasafiri hadi Mtwara kucheza na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
  Jumatatu Januari 30, 2017 kutakuwa na mchezo mwingine kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YAMSHUKURU RAIS DK. MAGUFULI KUUFUNGULIA UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top