• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 26, 2017

  ZULU YUPO FITI KUICHEZEA YANGA DHIDI YA MWADUI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Zambia, Justin Zulu yuko fiti kabisa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumapili dhidi ya Mwadui FC, Dar es Salaam.
  Yanga watakuwa wenyeji wa Mwadui FC katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumapili mjini Dar es Salaam, wakihitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao.
  Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online leo kwamba kwa sasa kwenye kikosi chao hakuna majeruhi kufuatia kupona kwa Zulu na kiungo mwingine Mzambia, Obrey Chirwa.
  Justin Zulu yuko fiti kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumapili dhidi ya Mwadui FC 

  Pamoja na hayo, Hafidh alisema mchezaji pekee ambaye atakosekana kwenye mchezo wa Jumapili ni mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye yuko kwao matatizo ya kifamilia.
  “Ni mchezaji mmoja tu ambaye hatupo naye hapa kwa sababu yupo kwao kwa matatizo ya kifamilia, Ngoma. Ila wengine wote wapo na wanaendelea na mazoezi.  
  Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea wikiendi hii, leo Mbao FC wakiwakaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kesho Simba SC wakiikaribisha Azam FC Uwanja wa Uhuru.
  Mechi nyingine za kesho, Tanzania Prisons wataikaribisha Mbeya City Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Toto Africans wataikaribisha African Lyon CCM Kirumba, Mwanza na Ndanda FC na  Maji Maji FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
  Jumapili mbali na Yanga kuwa wenyeji wa Mwadui FC, Kagera Sugar nao watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar na JKT Ruvu wataikaribisha Stand United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZULU YUPO FITI KUICHEZEA YANGA DHIDI YA MWADUI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top