• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 23, 2017

  MECHI YA SIMBA NA YANGA YASOGEZWA MBELE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya mahasimu, Simba na Yanga umesogezwa mbele hadi Februari 25, kutoka Februari 18, mwaka huu.
  Habari kutoka ndani ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba sababu ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni muingiliano na Ratiba ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.
  Februari 10, mwaka huu, Yanga watakuwa wageni wa Ngaya FC katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mde mjini Mde nchini Comoro, kabla ya kurudiana Februari 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kwa sababu hiyo, mchezo wa Simba na Yanga usingeweza kufanyika tena Februari 18 na busara za TFF zimeupeleka hadi Februari 25.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI YA SIMBA NA YANGA YASOGEZWA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top