• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 24, 2017

  SIMBA MEZANI NA OMAN CLUB BIASHARA YA BLAGNON

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  OMAN Club imeingia kwenye mazungumzo na Simba juu ya biashara ya mshambuliaji Muivory Coast, Frederick Blagnon.
  Katibu wa Simba, Patrick Kahemele aliiambia Bin Zubeiry Sports - Online jana kwamba Oman Club imeonyesha nia thabiti ya kumtaka mchezaji huyo na tayari mazungumzo yameanza.
  “Mazungumzo kati ya Simba na Oman Club yamenza na yanaendelea vizuri kuhusu Blagnon na sisi hatuna kipingamizi, tunachotaka ni kufanya biashara yenye faida,”alisema.
  Frederick Blagnon yuko mbioni kujiunga na Oman Club baada ya kushindwa kung'ara Simba

  Blagnon aliondoka wiki iliyopita kwenda kwao Ivory Coast na baadaye Oman kwa ajili ya mipango ya kujiunga na Fanja SC, ambayo hata hivyo ikazidiwa ujanja na Oman Club.
  Balgnon alisajiliwa Julai mwaka jana kutoka African Sports ya kwao, Ivory Coast kwa dau la Sh. Milioni 100, lakini ameshindwa kuonyeshwa umuhimu wake kwenye timu hiyo.
  Wakati huo huo: Simba SC inaingia kambini leo Ndege Beach, eneo la Mbweni, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Januari 28, mwaka huu.
  Kahemele alisema jana kwamba wachezaji wote wa Simba wanakwenda kambini kujiandaa na mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Jumamosi wiki hii.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA MEZANI NA OMAN CLUB BIASHARA YA BLAGNON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top