• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 30, 2017

  MBWANA MATUMLA KUREJEA ULINGONI MWEZI UJAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BINGWA wa zamani wa dunia wa ngumi za kulipwa uzito wa Bantam, Mbwana Ally Matumla anatarajiwa kurejea ulingoni mwezi ujao baada ya kupumzika kwa muda mrefu.
  Matumla, enzi zake akiitwa Golden Boy atapanda ulingoni Februari 5, mwaka huu Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam atakapopambana na Suleiman Shaaban katika pambano la raundi nane uzito wa Super Feather.
  Mbwana Ally Matumla anatarajiwa kurejea ulingoni mwezi ujao baada ya kupumzika kwa muda mrefu

  Mara ya mwisho Mbwana alipanda ulingoni Desemba 25, mwaka 2012 na kumpiga David Chalanga wa Kenya ukumbi wa Dar Live, Mbagala.
  Pambano hilo litatanguliwa na mapambano kadhaa ya utangulizi yakiwemo kati ya Meshack Mwankemwa na Ramadhani Shauri, Mohammed Matumla na Mfaume Mfaume, Twalibu Tuwa na Said Chino na Hussein Pendeza na Said Hamdan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBWANA MATUMLA KUREJEA ULINGONI MWEZI UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top