• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 23, 2017

  SAMATTA AFIKISHA MABAO 10 MWAKA MMOJA KRC GENK

  Na Mwandishi Wetu, DAE ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa juzi alifunga bao lake la kwanza mwaka huu na la 10 tangu ajiunge na KRC Genk ya Ubelgiji. 
  Samatta alifunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya As Eupen kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Kehrweg mjini Eupen.
  Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, ijulikanayo kama Taifa Stars kwa jina la utani, alifunga bao hilo dakika ya 82 akimalizia pasi ya kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy.
  Mbwana Samatta akiwa amebebwa juu na wenzake baada ya kufunga bao muhimu ugenini juzi 
  Hilo linakuwa bao lake la kwanza msimu huu na la 10 tangu ajiunge na Genk mwaka mmoja sasa

  Huo ulikuwa mchezo wa 37 kwa Samatta tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 19 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 18 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na nane msimu huu.
  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati nane hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na mbili msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 10, manne msimu huu na sita msimu uliopita.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot, Uronen, Colley, Dewaest, Castagne, Heynen/Berge dk45 Malinovskyi, Pozuelo, Trossard/Writers dk60, Bailey na Samatta.
  AS Eupen: Crombrugge Al-Abdulrahman, Blondelle, Diallo, Wague/Cases dk84, Diagne, Luis Garcia, Lazare, Ocansey/Bassey dk65, Onyekuru na Mamadou.
  VIDEO SAMATTA AKIZUNGUMZA BAADA YA MECHI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AFIKISHA MABAO 10 MWAKA MMOJA KRC GENK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top