• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 29, 2017

  TIMU YA SAMATTA YACHEZEA KICHAPO UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana ameshindwa kuinusuru KRC Genk kuchapwa 1-0 na KV Mechelen katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji. 
  Samatta alicheza kwa dakika zote 90 jana Uwanja wa ugenini wa AFAS Achter de Kazerne mjini Mechelen na bao pekee la beki Mbelgiji, Seth De Witte dakika ya 89 likawapa wenyeji ushindi wa 1-0.
  Mbwana Samatta akimuacha chini beki wa wapinzani jana
  Samatta akiwania mpira wa juu dhidi ya mchezaji wa KV Mechelen
  Samatta akiondoka na mpira mbele ya mchezaji wa KV Mechelen
  Samatta akipiga shuti mbele ya mchezaji wa KV Mechelen

  Kuna wakati Samatta alianguka na akashika mdomo kama ameumizwa meno

  Huo ulikuwa mchezo wa 39 kwa Samatta tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 21 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 20 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tisa msimu huu.
  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati tisa hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 11, matano msimu huu na sita msimu uliopita.
  Kikosi cha KV Mechelen kilikuwa: Coosemans, Paulussen, El Messaoudi, White, Croizet/Matthys dk71, Zipper, Bjelica, Kolovos/Verdier dk62, Van Cleemput, Vanlerberghe na Claes.
  KRC Genk : Jackers, Wouters, Colley, Dewaest, Castagne/Walsh dk33 Heynen, Malinovskyi/Berge dk80, Pozuelo/Naranjo dk93 Trossard, Authors na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIMU YA SAMATTA YACHEZEA KICHAPO UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top