• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 26, 2017

  KOCHA MPYA AZAM AJA NA MBINU MPYA ZA KUIUA SIMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Aristica Cioaba, amekuja na mbinu mpya ya kuwapa motisha wachezaji wanaocheza kwenye timu inayofanya vizuri mazoezini.
  Mbinu hiyo imeanza kutumika kwenye mazoezi ya leo asubuhi ya timu hiyo katika maandalizi ya kuelekea mchezo na Simba, ambapo Mromania huyo aliweka mezani kitita cha Sh. 100,000 kugombewa na timu zitakazofanya vizuri mazoezini.
  Cioaba aliwagawa wachezaji wake katika timu nne zenye wachezaji sita kila moja na kuanza kucheza mechi za wenyewe kwa wenyewe na hatimaye timu iliyokuwa ikiongozwa na kipa Aishi Manula, ikafanikiwa kuibuka kidedea kwa kuzifunga timu zote tatu walizocheza nazo na kuzoa kitita cha Sh. 60,000.
  Wachezaji wengine waliokuwa kwenye timu hiyo ni mabeki Gadiel Michael, Daniel Amoah, viungo Mudathir Yahya, Stephan Kingue na mshambuliaji Yahaya Mohammed, ambao kila mmoja kwenye timu hiyo aliambulia Sh. 10,000 katika mgawanyo wa kiasi hicho.
  Kiasi kingine cha fedha kilichobakia Sh. 40,000 kilikosa mshindi kufuatia timu zingine tatu zilizobakia kila mmoja kulingana na mwenzake kwa ushindi wa idadi ya mechi walizocheza.
  Kocha huyo ametumia mbinu hiyo kwenye mazoezi kama sehemu ya kuwawekea motisha wachezaji kufanya mazoezi kwa bidii na nguvu ili kujiandaa vema na mechi zinazokuja, na hiyo iliwafanya wachezaji kuyafurahi mazoezi na kuwaongezea zaidi ushindani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA MPYA AZAM AJA NA MBINU MPYA ZA KUIUA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top