• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 26, 2017

  MBEYA CITY WAPANIA KUISAMBARATISHA PRISONS

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  BAADA ya  ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Kabela City FC ya Shinyanga kwenye kombe la FA hapo jana, kikosi cha Mbeya City Fc leo kimeanza mazoezi kujindaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prison  uliopangwa  kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.
  Kocha  Msaidizi wa kikosi hiki Mohamed Kijuso amesema kwamba maandalizi kuelekea mchezo  huo wa Jumamosi yanaenda vizuri na wachezaji wote wako kwenye hali nzuri, kinachofanyia  sasa ni kurekebisha makosa  yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kombe la FA licha ya kupatikana kwa ushindi wa bao 2-0.
  "Tunashukuru Mungu  kwa sababu tulipata matokeo kwenye mchezo wa kombe la FA hapo jana licha ya mchezo kuwa mgumu, tuko mazoezini hivi sasa kurekebisha makosa yote yalitokea  hii ni sehemu ya maandalizi yetu kuelekea mchezo ujao,"alisema.
  Kijuso aliongeza kuwa kwa mujibu wa daktari, vijana wachezaji wote wapo fiti kuelekea mchezo huo. "Ninaiheshimu Tanzania Prison ni timu nzuri  huwezi kuibeza kwa namna yoyote,  ni wazi mchezo wa jumamosi utakuwa mgumu,".
  Akiendelea  zaidi Kijuso alisema kuwa mipango na malengo ya kikosi chache ni kuhakikisha   wanakuwa sehemu ya timu nne za juu kwenye msimamo wa ligi  mara ifikapo mwisho wa msimu.
  Mara kadhaa nimekuwa nikisema nia  yetu ni kuwa  sehemu ya timu nne za juu mwisho wa msimu,hili litawezekana kwa sababu nafasi bado tunayo, nina imani kubwa na vijana wangu kwa sababu sasa wako kwenye kiwango kizuri, kitu pekee naomba mashabiki wetu  watusapoti kwa nguvu zote kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwenye michezo iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY WAPANIA KUISAMBARATISHA PRISONS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top