• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 29, 2017

  MANE AKOSA PENALTI, CAMEROON YAING'OA SENEGAL KWA MATUTA

  TIMU ya Cameroon usiku wa jana imeifunga Senegal kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 na kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon.
  Katika mchezo huo mkali wa Robo Fainali uliopigwa Uwanja wa Franceville, mji mkuu wa Gabon, Franceville Senegal walitawala mchezo mwanzoni na kuwafanya Cameroon wacheze kwa kujihami zaidi.
  Lakini mambo yakabadilika na baadaye Simba wa Teranga wakajikuta wanapunguza kasi yao na kuwap mwanya Simba Wasiofungika.
  Sadio Mane alikosa penalti ya mwisho jana Cameroon ikiitoa Senegal kwa penalti 5-4

  Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane ambaye alikuwa shujaa wa Senegal wakati wote kwenye mashindano jana alikosa penalti ya mwisho baada ya mkwaju wake kuokolewa na kipa Ondoa na Cameroon ikashinda kwa penalti 5-4.
  Waliofunga penalti za Cameroon ni Moukandjo, Oyongo, Teikeu, Zoua na Aboubakar wakati za Senegal zilifungwa na Koulibaly, Kara, Sow na Saivet.
  Kikosi cha Senegal kilikuwa: Diallo, Mbodji, Koulibaly, Mbengue/Ciss dk85, Gassama, Gueye, Kouyate/Ndiaye dk110, Saivet, Diouf/Sow dk65, Mane, Balde.
  Cameroon: Ondoa, Fai, Teikeu, Ngadeu, Oyongo, Siani, Djoum/Mandjeck dk102, Moukandjo, Toko Ekambi/Zoua dk47, Tambe/Aboubakar dk102 na Bassogog.
  Katika Robo Fainali ya kwanza, mabao mawili ya Aristide Bance na Prejuce Nakoulma kipindi cha pili yalitosha kuipa Burkina Faso ushindi wa 2-0 dhidi ya Tunisia jana Uwanja wa d'Angondjé mjini Libreville na kwenda Nuu Fainali.
  Robo Fainali za mwisho zinachezwa leo kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Ghana Uwanja wa d'Oyem Saa 1:00 usiku na Misri na Morocco Uwanja wa Port Gentil Saa 4:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANE AKOSA PENALTI, CAMEROON YAING'OA SENEGAL KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top