Na Mwandishi Wetu, KAMPALA
WACHEZAJI wa Uganda wamezawadiwa dola za Kimarekani 1,000 sawa na Sh. Milioni 2 za Tanzania kila mmoja baada ua kuifunga mabao 2-0 Botswana katika mchezo wa ufunguzi Fainali za Mataifa ya Afrika juzi.
Zawadi hiyo ilikuwa ahadi ya Rais wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Mhandisi Moses Magogo aliyeitoa wiki iliyopita wakati alipokutana na wachezaji katika hoteli ya Sky iliyopo Nalya.
Ahadi hiyo ilitimizwa Jumamosi hiyo hiyo wakati wachezaji 18 walioshiriki mchezo huo, walipopewa jumla ya dola 18,000 wakati wachezaji wengine ambao hawakuvaa jezi, lakini walikuwapo kambini, kila mmoja alipewa kifuta jasho cha dola 500.
Mara tu baada ya mechi, Rais wa FUFA, Injinia Magogo alizungumza na wachezaji wa timu hiyo inayofundishwa na kocha Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ katika chumba cha kubadilishia nguo.
Rais wa FUFA akawapongeza wachezaji kwa mwanzo mzuri kwenye mbio za AFCON 2017, akisema; “Hizi ni kampeni za mbio ndefu. Tuna mechi tano zaidi za kucheza. Unatakiwa kuripoti tena mara moja utakapopata ruhusa ya klabu yako. Acha tupongeze klabu kwa kazi nzuri ya kuwaruhusu kwa majukumu ya kitaifa,”amesema Magogo.
Mfungaji wa bao la kwanza la Korongo wa Uganda juzi, Geoffrey Massa alisema analitoa bao lake kwa binti yake, Judith Massa ambaye alikuwa anatimiza miaka saba Juni 5.
“Nilimuahidi Judith sherehe nzuri za kuzaliwa kwake kwa kuifungia bao Uganda Cranes. Nina furaha nimetimiza ahadi yangu kwa Judith”alisema Massa.
Brian Umony ambaye alifunga bao la pili, amesema kwamba amefurahia mwanzo mzuri akichangia timu kuvuna pointi tatu. Uganda itarudi tena kwenye mbio za AFCON 2017 Septemba 5 mwaka huu itakaposafiri kwenda Moroni kuwafuata Comoro.

![]() |
| Kikosi cha Uganda ambacho Jumamosi kiliifunga Botswana 2-0 Uwanja wa Taifa wa Mandela, Kampala |
Mara tu baada ya mechi, Rais wa FUFA, Injinia Magogo alizungumza na wachezaji wa timu hiyo inayofundishwa na kocha Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ katika chumba cha kubadilishia nguo.
Rais wa FUFA akawapongeza wachezaji kwa mwanzo mzuri kwenye mbio za AFCON 2017, akisema; “Hizi ni kampeni za mbio ndefu. Tuna mechi tano zaidi za kucheza. Unatakiwa kuripoti tena mara moja utakapopata ruhusa ya klabu yako. Acha tupongeze klabu kwa kazi nzuri ya kuwaruhusu kwa majukumu ya kitaifa,”amesema Magogo.
Mfungaji wa bao la kwanza la Korongo wa Uganda juzi, Geoffrey Massa alisema analitoa bao lake kwa binti yake, Judith Massa ambaye alikuwa anatimiza miaka saba Juni 5.
“Nilimuahidi Judith sherehe nzuri za kuzaliwa kwake kwa kuifungia bao Uganda Cranes. Nina furaha nimetimiza ahadi yangu kwa Judith”alisema Massa.
Brian Umony ambaye alifunga bao la pili, amesema kwamba amefurahia mwanzo mzuri akichangia timu kuvuna pointi tatu. Uganda itarudi tena kwenye mbio za AFCON 2017 Septemba 5 mwaka huu itakaposafiri kwenda Moroni kuwafuata Comoro.

.png)
0 comments:
Post a Comment