• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 24, 2015

  ETO’O AENDA KUMALIZIA SOKA YAKE ‘KITIMU’ KILICHOPANDA DARAJA UTURUKI

  MWANASOKA bora wa zamani Afrika, Samuel Eto'o (pichani) ameripotiwa kukubali kuhamia timu iliyopanda Ligi Kuu ya Uturuki, Antalyaspor.
  Klabu hiyo imethibitisha kwamba imefikia makubaliano na Eto'o, lakini Mkataba bado haujasainiwa kwa sababu tatizo la haki za matumizi ya picha za mkongwe huyo wa Cameroon nchini Italia bado halijatatuliwa.
  "Tuna makubaliano na mchezaji. Lakini kuna matatizo fulani kuhusu haki za matumizi ya picha za mchezaji Italia. Tutatatua matatizo hayo haraka iwezekanavyo,” imesema klabu hiyo ya Uturuki.
  Tayari gazeti la Gazzetta dello Sport la Italia limeripoti kwamba Rais wa Sampdoria, Massimo Ferrro anaamini mkali huyo wa mabao wa kihistoria Afrika mwenye umri wa miaka 34 ataondoka kiasi cha miezi sita tangu arejee Italia.
  Ferrero amesema kuondoka kwa Eto'o ni "matakwa ya nafsi yake na pochi yake ya fedha."
  Mkali huyo wa mabao wa zamani wa Cameroon kwa sasa anamalizia soka yake baada ya kutamba klabu kubwa kama FC Barcelona, Inter Milan, Chelsea na Everton.
  Eto'o ni mshindi wa mataji mawili Mataifa ya Afrika, moja la Serie A, matatu ya La Liga titles, Meda,I ya Dhahabu ya Olimpiki na mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Mshambuliaji huyo alitua Sampdoria Januari, lakini ameweza kufunga mabao mawili tu katika mechi 18 alizochezea The Blucerchiati.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ETO’O AENDA KUMALIZIA SOKA YAKE ‘KITIMU’ KILICHOPANDA DARAJA UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top