• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 29, 2015

  SIMBA SC YASHUSHA MZUNGU MWINGINE, HATARI TUPU MSIMBAZI

  KATIKA mkakati endelevu wa kuboresha benchi la ufundi, Klabu ya Simba imeingia mkataba na Dusan Momcilovic (pichani) kama kocha mpya wa mazoezi ya viungo na anatarajiwa kuanza kazi rasmi mwanzoni mwa mwezi July.
  Tovuti ya Simba SC imeandika; "Kocha huyo kutoka Nchini Serbia ana uzoefu mkubwa katika fani ya mpira wa miguu hususani mazoezi ya viungo. Kocha Dusan amefundisha klabu mbalimbali duniani kwenye Nchi kama Malaysia, Indonesia, Georgia ambako Alikuwa kocha wa mazoezi ya viungo wa klabu ya FC DINAMO ambayo ilicheza mechi za awali ya klabu bingwa ya Ulaya-UEFA, Bosnia na Herzegovina, Oman na Belgrade,"
  Imeeleza kwamba Kocha Dusan pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu ya FC SOGOR –Tobruk – Libya.
  Kocha Dušan ni muhitimu wa Digrii ya Mazoezi ya Viungo jijini Belgrade akiwa amejikita Zaidi kwenye mazoezi ya viungo na kujenga mwili.
  "Klabu ya Simba inafuraha kubwa kuingia mkataba na kocha Dusan Momcilovic mwenye uzoefu na weledi wa kutosha, tunaamini atakuwa chachu ya mafanikio pia kunoa vipaji vya wachezaji wa Simba." imeandika tovuti ya Simba.
  Kocha Mkuu wa Simba SC ni Muingereza Dylan Kerr, Msaidizi wake mzalendo Suleiman Matola wakati kocha wa makipa ni Abdul Iddi Salim.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASHUSHA MZUNGU MWINGINE, HATARI TUPU MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top