• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 23, 2015

  YANGA SC KUCHEZA NA FRIENDS RANGERS KESHO KARUME, BOBAN NDANI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC kesho asubuhi watacheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Friends Rangers ya Magomeni Kagera Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
  ‘Bosi’ wa Rangers, Heri Mzozo ameiambia BIN ZUBEIRY leo Dar es Salaam kwamba kwao, mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
  Mzozo amesema kwamba pamoja na wachezaji walioichezea timu hiyo msimu uliopita, Rangers pia imewaalika baadhi ya wachezaji ambao waliibukia kwao au wamewahi kuchezea timu hiyo kabla ya kwenda kutamba timu nyingine.
  Amewataja baadhi ya wachezaji hao ni pamoja na Haruna Moshi ‘Boban’, Juma Nyoso, Jabir Aziz, Rashid Mandawa, Mahundi, Credo Mwaipopo, Yussuf Mgwao, Amir Maftah, Stanley Nkomola, Mussa John ‘Rooney’, Hassan Hatibu na wengineo.
  Kwa Yanga SC, mchezo huo utakuwa wa kukiangalia kikosi chake kabla ya kumenyana na SC Villa ya Uganda mwishoni mwa wiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC KUCHEZA NA FRIENDS RANGERS KESHO KARUME, BOBAN NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top