• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 25, 2015

  ARSENAL YASAJILI KIUNGO KINDA MROMANIA MWENYE KIPAJI CHA AJABU

  KLABU ya Arsenal ipo kwenye hatua za mwishoni kukamilisha usajili wa kinda wa miaka 16 mwenye kipaji cha ajabu, Vlad Dragomir.
  Dragomir ameonekana katika picha akiwa na Mkuu wa MIjadala wa Arsenal, Dick Law Jumatano na kiungo huyo ambaye anatokea ACS Poli Timisoara, atasaini Mkataba wa miaka mitatu Emirates.
  Nahodha huyo wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Romania, pia amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na Inter Milan na Monaco, lakini Gunners imekuwa bahati yao kinda huyo.
  Arsenal should complete the signing of 16-year-old wonderkid Vlad Dragomir (pictured with Dick Law, right)
  Vlad Dragomir (katikati) akiwa na Dick Law kulia

  Inaaminika Dragomir, ambaye alitimiza miaka 16 Aprili 24, mwaka huu, amevutiwa zaidi na The Gunners kutokana na sera yao ya kuwapa nafasi vijana wadogo kuonyesha vipaji vyao katika timu ya kwanza. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YASAJILI KIUNGO KINDA MROMANIA MWENYE KIPAJI CHA AJABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top