• HABARI MPYA

    Friday, June 26, 2015

    VIFAA VIWILI VYATUA YANGA SC KESHO, NI ZUTAH NA NGOMA

    Joseph Tetteh Zutah anatua kesho Yanga SC
    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KIUNGO chipukizi wa Ghana, Joseph Tetteh Zutah na mshambuliaji wa Zimbabwe, Donald Ngoma kwa pamoja wanawasili kesho nchini kwa ajili ya kuja kujiunga na Yanga SC.
    Zutah aliyezaliwa Agosti 22, mwaka 1994 anatokea klabu ya Medeama ya kwao, wakati Ngoma anatokea FC Platinum ya kwao pia na wote watafika asubuhi.
    Yanga SC imekwishafanya mazungumzo ya awali na wachezaji hao na wanatarajiwa kuja kusaini mikataba.
    Yanga SC iliitoa Platinum katika hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu, lakini kocha Mholanzi Hans van der Pluijm akavutiwa mno na Ngoma, aliyecheza mechi moja tu ya Zimbabwe baada ya kukosa mechi ya Dar es Salaam kwa sababu alikuwa majeruhi.
    Na Pluijm ambaye amewahi kufundisha Ghana, ndiye aliyempendekeza Zutah ambaye uongozi wa Yanga SC haujawahi kumuona kabisa, lakini vyanzo vinasema huyo ni mchezaji mzuri anayeweza kucheza pia kama beki wa kulia.
    Akiwa na umri wa miaka 26, Ngoma ni mchezaji mwenye uwezo na uzoefu mkubwa, kwani amekwishaichezea Zimbabwe hadi kwenye Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).
    Donald Ngoma anawasili kesho Yanga SC

    Januari 2014, kocha Ian Gorowa alimuorodhesha Ngoma katika kikosi cha Zimbabwe ambacho kilimaliza katika nafasi ya nne CHAN baada ya kufungwa na Nigeria 1-0 katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu mwaka jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VIFAA VIWILI VYATUA YANGA SC KESHO, NI ZUTAH NA NGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top