• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 30, 2015

  KIIZA AJIFUNGA MIAKA MIWILI SIMBA SC

  Hamisi Kiiza (kushoto) akiwa na Emmanuel Okwi (kulia)
  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga SC, Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’ atawasili nchini wakati wowote kusaini Mkataba wa miaka miwili kuwatumikia Simba SC.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba wamefikia makubaliano na Mganda huyo kuja kusaini Msimbazi.
  “Sisi na Kiiza kila kitu safi, anakuja kusaini miaka miwili hapa,”alisema.
  Kiiza aliachwa na Yanga SC Desemba mwaka jana, baada ya kuitumikia klabu hiyo tangu mwaka 2011. Na aliachwa ili asajiliwe mshambuliaji Mliberia, Kpah Sherman.
  Mganda huyo mkali wa mabao tangu hapo amekuwa hana timu, baada ya mpango wake wa kwenda kucheza Fanja ya Oman kushindikana Januari mwaka huu.
  Sasa Kiiza anarejea Tanzania, lakini si mitaa ya Jangwani tena, bali Msimbazi yalipo maskani ya Simba SC.  
  Akisajiliwa Kiiza atafanya Simba SC iwe na wachezaji watano wa kigeni, wengine wakiwa ni Waganda wenzake, beki Juuko Murushid, washambuliaji Simon Sserunkuma na Emmanuel Okwi na Mrundi Laudit Mavugo.
  Maana yake Simba SC ina nafasi mbili zaidi kwa ajili ya wachezaji wa kigeni, huku ikielezwa kuna beki Mrundi wamekwishamalizana naye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIIZA AJIFUNGA MIAKA MIWILI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top