• HABARI MPYA

    Monday, June 15, 2015

    ‘MIDO’ LA YANGA SC KIPENZI CHA BRANDTS LATUA AFRICAN SPORTS MWAKA MMOJA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    AFRICAN Sports imemsajili kiungo wa zamani a Yanga SC, Bakari Masoud kwa Mkataba wa mwaka mmoja.
    ‘Baker’ amesajiliwa Sports iliyopanda tena Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutoka Fanja FC ya Oman aliyoichezea kwa msimu uliopita.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo Dar es Salaam, Baker amesema kwamba amechagua kusaini Sports kwa sababu Tanga ni nyumbani kwao na anaamini huko atapata nafasi ya kucheza na kukuza kiwango chake.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, alitua Yanga SC mwaka 2013, akitokea Coatsal Union ya Tanga pia, ambayo ilimpandisha kutoka timu yake ya vijana.
    Bakari Masoud alipokuwa Uturuki na Yanga SC mwaka juzi
    Bakari Masoud akisaini Africa Sports ya Tanga
    Bakari Masoud akiwa na wachezaji wa Fanja mjini Muscat

    Tunda hilo la Makorola Academy, Tanga lilikuwa kipenzi cha kocha wa zamani wa Yanga SC, Mholanzi Ernie Brandts ambaye alitimuliwa Yanga SC Desemba mwaka juzi.
    Baker alikuwemo kwenye kikosi cha Yanga SC kilichokwenda Uturuki mwaka juzi kwa ziara ya mafunzo- lakini baada ya Brandts kuondoka timu hiyo ya Jangwani, Dar es Salaam, thamani yake ikashuka naye akaondoka.
    Alikwenda Malaysia ambako baada ya muda akatimkia Fanja alipocheza msimu uliopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ‘MIDO’ LA YANGA SC KIPENZI CHA BRANDTS LATUA AFRICAN SPORTS MWAKA MMOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top