• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 29, 2015

  OKWI 'ALIPOJIBEBEA JUMLA' KIMWANA FLORENCE NAKALEGGA, WENYE WIVU WAJINYONGE!

  Okwi akifurahia na mkewe Florence wakati wa ndoa yao
  MSHAMBULIAJI wa Simba na timu ya Taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi amefunga ndoa na Florence Nakalegga wikiendi iliyopita. Harusi hiyo ya kufana ilifanyika jijini kampala kwenya kanisa la Rubaga Miracle Center Church ilifungishwa na mchungaji Robert.
  Tovuti ya Simba SC imeandika kwamba harusi hiyo ya kufana ilihudhuriwa na wadau wengi wa soka, watu maarufu na viongozi mbalimbali wa jiji la Kampala na Uganda. Msimamizi wa harusi hiyo alikuwa ni Hamisi Kiiza ambaye ni rafiki yake wa siku nyingi na mchezaji wa zamani wa Yanga SC.
  "Uongozi wa Simba Sports Club unamtakia kila la kheri Bibi na Bwana Emmanuel Okwi kwenye maisha yao mapya ya ndoa,"imeandika tovuti hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: OKWI 'ALIPOJIBEBEA JUMLA' KIMWANA FLORENCE NAKALEGGA, WENYE WIVU WAJINYONGE! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top