• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 28, 2015

  SAMATTA NA ULIMWENGU WAANZIA BENCHI MAZEMBE IKITOA SARE NA HILAL

  Mbwana Samatta (kushoto) na Thomas Ulimwengu wote wameanzia benchi leo Mazembe ikilazimishwa sare ya 0-0 El Hilal mjini Lubumbashi
  WENYEJI TP Mazembe wamelazimishwa sare ya bila kufungana na El Hilal ya Sudan jioni ya leo katika mchezo wa kwanza wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi.
  Na sare hiyo Mazembe wameshukuru, kwani kipa wao mkongwe Muteba Kidiaba aliokoa mchomo wa hatari dakika za lala salama.
  Baada ya kosakosa nyingi, kocha wa Mazembe, Patrice Carteron alimuingiza mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Samatta kuchukua nafasi ya Mzambia, Given Singuluma mapema kipindi cha pili ambaye alikwenda kuipa wakati mgumu safu ya ulinzi ya Hilal inayoundwa na wakali kama Nahodha Saif Eldin Masawi, Atir Magor na Muawia Bashir.
  Mtanzania mwenzake Samatta, Thomas Ulimwengu aliingia pia baadaye kipindi cha pili, lakini tayari Mazembe walikuwa ‘wamekwishashikwa’ na hakuweza kusaidia kubadilisha matokeo.
  Sasa timu zinaanza na pointi moja kila moja, kabla ya mchezo mwingine wa Kundi A kati ya Smouha ya Misri na Moghreb Tetouane ya Morocco baadaye usiku huu mjini Alexandria.
  Matokeo ya mechi za awali za Kundi B juzi El Merreikh ya Sudan ilishinda 2-0 nyumbani dhidi ya MC Eulma ya Algeria, wakati jana ES Setif ilifungwa 2-1 na Waalgeria wenzao, USM Alger.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA NA ULIMWENGU WAANZIA BENCHI MAZEMBE IKITOA SARE NA HILAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top