• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 23, 2015

  SOMOE AWANIA UKATIBU MSAIDIZI CHAMA CHA SOKA YA WANAWAKE TANZANIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWANDISHI Mwandamizi wa michezo wa gazeti la NIPASHE, Somoe Ng'itu (pichani) leo amechukua fomu kuwania nafasi ya Katibu Msaidizi katika uchaguzi mdogo wa  Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA).
  Somoe amechukua fomu leo Jumanne mchana na kuirejesha jioni kutokana na siku hiyo kuwa ya mwisho katika zoezi hilo.
  TWFA inatarajia kufanya uchaguzi huo mdogo kujaza nafasi nne zilizotangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya chama hicho ambayo ilisema kwamba uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 15 mwaka huu.
  Nafasi zinazotarajiwa kujazwa katika uchaguzi huo ni pamoja na ya Mwenyekiti, Katibu Msaidizi na nyingine mbili za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
  Nafasi ya Mwenyekiti imebakia wazi baada ya aliyekuwa kiongozi katika nafasi hiyo, Lina Kessy kupata ajira nchini Ethiopia na hivyo kukosa muda wa kufanya shughuli za TWFA.
  Chama hicho ni chama shirikishi na viongozi wake watatu hupata nafasi ya kuingia katika Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SOMOE AWANIA UKATIBU MSAIDIZI CHAMA CHA SOKA YA WANAWAKE TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top