• HABARI MPYA

    Saturday, June 20, 2015

    TFF YAPITISHA WACHEZAJI SABA WA KIGENI LIGI KUU NA WOTE WANACHEZA

    Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeongeza idadi ya wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kutoka watano hadi saba kuanzia msimu ujao.
    Hayo yaamepitishwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika kuanzia Saa 3:00 asubuhi hadi Saa 11:30, ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo, eneo la Kikwajuni, Zanzibar.
    Habari kutoka ndani ya kikao hicho, kilichoongozwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi zimesema kwamba pamoja na hayo, kila klabu italazimika kumlipia kila mchezaji ada ya dola za Kimarekani 2,000 (Sh. Milioni 4) kwa msimu.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi (katikati) akiongoza kikao cha Kamati ya Utendaji leo ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar, eneo la Kikwajuni visiwani humo leo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAPITISHA WACHEZAJI SABA WA KIGENI LIGI KUU NA WOTE WANACHEZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top