• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 26, 2015

  MKWASA AWAPIGA CHINI AGGREY MORRIS NA MKUDE TAIFA STARS

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  BEKI Vincent Andrew wa Mtibwa Sugar na kiungo Mudathir Yahya wa Azam FC wameongezwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2016 dhidi ya Uganda wiki ijayo mjini Kampala.
  Andrew amekwenda kuziba pengo la Aggrey Morris wa Azam FC ambaye ni majeruhi na Mufathir amekwenda kuchukua nafasi ya Jonas Mkude aliyekwenda kufanya majaribio klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini.
  Taifa Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja huo wa Boko Veterani, huku timu ikiweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo.
  Aggrey Morris (kulia) ameenguliwa kikosi cha Taifa Stars kwa sababu ya majeruhi na nafasi yake imechukuliwa na Vincent Andrew wa Mtibwa Sugar 

  Wachezaji 26 walioingia kambini jana kuanza maandalizi ya kwenda kupindua kipigo cha 3-0 wiki mbili zijazo mjini Kampala, Uganda ili kusonga mbele CHAN ni makipa; Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ali (Azam FC) na Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga) na mabeki ni Shomary Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC), Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC), Kevin Yondan (Yanga SC), Hassan Isihaka (Simba SC), Andrew Vincent (Mtibwa Sugar).
  Viungo ni Mudathir Yahya (Azam FC), Abdi Banda (Simba SC), Salum Telelea (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Simon Msuva (Yanga SC), Said Ndemla (Simba SC), Ramadhani Singano ‘Messi’ (Simba SC) na Deus Kaseke (Mbeya City).
  Washambuliaji ni John Bocco (Azam FC), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Ame Ali (Mtibwa Sugar), wakati wengine ambao wamewekwa akiba ni Juma Abdul wa Yanga SC, Mudathir Yahya wa Azam FC na Samuel Kamuntu wa JKT Ruvu.
  Mara baada ya kuteuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kurithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij aliyefukuzwa mwishoni mwa wiki kufuataia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Uganda katika mchezo wa kwanza na Uganda, Mkwasa alitaja benchi lake Ufundi, akimteua King Kibaden kuwa Mshauri wake wa Ufundi.
  Hemed Morocco kocha Msaidizi, Manyika Peter kocha wa makipa, Mtunza Vifaa ni Hussein Swedi ‘Gaga’, Meneja Juma Mgunda na Mratibu Msafiri Mgoyi, wakati Daktari atatajwa baadaye.
  Stars itaendelea kuwa kambini Kiromo na kufanya mazoezi Boko Veterani hadi itakaposafiri kwenda Uganda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MKWASA AWAPIGA CHINI AGGREY MORRIS NA MKUDE TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top