• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 24, 2015

  MKWASA ATEUA STARS MPYA, ‘AWAPA SHAVU’ KIBADEN, MANYIKA NA MGUNDA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KOCHA mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha timu hiyo pia akimteua gwiji Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ kuwa Mshauri wake wa Ufundi.
  Mkwasa ameteuliwa jana kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, akirithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij aliyefukuzwa mwishoni mwa wiki kufuataia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Uganda katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza kufuzu michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Rwanda.
  Na leo Mkwasa ameteua wachezaji 26 watakaoingia kambini Jumamosi kuanza maandalizi ya kwenda kupindua kipigo cha 3-0 wiki mbili zijazo mjini Kampala, Uganda ili kusonga mbele CHAN.
  Kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari leo. Kulia ni Msaidizi wake, Hemed Morocco

  Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam, Mkwasa amesema kwamba amemteua pia Manyika Peter kuwa kocha wa makipa.
  Amesema benchi lake la Ufundi linakamilishwa na Mtunza Vifaa, Hussein Swedi ‘Gaga’, Meneja Juma Mgunda na Mratibu Msafiri Mgoyi, wakati Daktari atatajwa baadaye.
  Mkwasa ametaja kikosi kipya cha Taifa Stars akimtema aliyekuwa kipa namba moja chini ya Nooij, Deo Munishi ‘Dida’, akiwachukua makipa watatu; Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ali (Azam FC) na Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga).
  Mabeki ni Shomary Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC), Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC), Kevin Yondan (Yanga SC), Hassan Isihaka Simba SC, Aggrey Morris (Azam FC).
  Viungo ni Jonas Mkude (Simba SC), Abdi Banda (Simba SC), Salum Telelea (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Simon Msuva (Yanga SC), Said Ndemla (Simba SC), John Bocco (Azam FC), Ramadhani Singano ‘Messi’ Simba SC na Deus Kaseke (Mbeya City).
  Washambuliaji ni Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Ame Ali (Mtibwa Sugar), wakati wengine ambao wamewekwa akiba ni Juma Abdul wa Yanga SC, Mudathir Yahya wa Azam FC na Samuel Kamuntu wa JKT Ruvu.
  Kesho, benchi la Ufundi la Stars litakutana na wachezaji wote walioteuliwa katika hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, Dar es Salaam kuwaelimisha juu ya uzalendo na Mkwasa amesema Jumamosi timu itaenda kuweka kambi nje ya mji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MKWASA ATEUA STARS MPYA, ‘AWAPA SHAVU’ KIBADEN, MANYIKA NA MGUNDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top