• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 22, 2015

  ADEBAYOR AAMUA KUBAKI SPURS BAADA YA 'KUWATUNGUA' LIBERIA

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor amesema kwamba ana hamu ya kuwaonyesha mashabiki wa Tottenham mapenzi yake kwa klabu hiyo kuelekea matayarisho ya msimu mpya.
  Ilikuwa inafikiriwa kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ataondoka White Hart Lane msimu huu baada ya kutokuwa na msimu mzuri uliopita wa Ligi Kuu England.
  Adebayor alifunga mabao mawili tu katika mechi 17 alizoichezea timu hiyo ya Kaskazini mwa London msimu uliopita, kati ya hizo tisa tu ndiyo alianza kwenye kikosi cha Mauricio Pochettino.

  Emmanuel Adebayor alitarajiwa kuondoka Spurs, lakini sasa amesema anabaki London Kaskazini

  West Ham ilijaribu kumsajili kwa mkopo 'Ade Mabao' Januari, lakini Mwenyekiti wa klabu hiyo, Daniel Levy akagoma na baada ya Adebayor kuifungia Togo bao la ushindi dhidi ya Liberia wiki iliyopita mechi za kufuzu AFCON, ameibuka.
  Adebayor, ambaye analipwa karibu Pauni 100,000 kwa wiki katika klabu hiyo, ametweet mwishoni mwa wiki: "Najisikia freshi haswa baada ya bao langu. Nina hamu yab kurejea Tottenham na kumuonyesha kila mmoja mapenzi niliyonayo kwa klabu. Nasonga mbele kwenye maandalizi ya msimu mpya!" 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ADEBAYOR AAMUA KUBAKI SPURS BAADA YA 'KUWATUNGUA' LIBERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top