• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 24, 2015

  KIONGERA ATUA DAR KUJIUNGA NA SIMBA SC, DAKTARI ASEMA; “GOTI LAKE BADO BADO”

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Mkenya wa Simba SC, Paul Mungai Kiongera atahitaji mwezi wa mapumziko kabla ya kuanza tena kuichezea timu hiyo.
  Tovuti ya Simba SC imeandika leo kwamba, Kiongera aliwasili jana nchini na kufanyiwa vipimo, ambavyo vimegundua kwamba anahitaji mwezi mmoja wa zaidi wa mapumziko.
  “Vipimo hivyo vya afya vilifanyika leo saa tano asubuhi na baada ya vipimo Daktari wa timu alishauri Kiongera kupewa mapumziko ya mwezi mmoja kabla ya kujiunga na timu rasmi,”imeandika tovuti rasmi ya Simba SC.
  Paul Kiongera atahitaji mwezi mmoja wa mapumziko kabla ya kuanza mazoezi Simba SC

  Kiongera alisajiliwa Simba SC msimu uliopita kutoka KCB ya kwao, Kenya lakini baada ya wiki tatu akatonesha goti lake na kwenda kufanyiwa upasuaji India.
  Kwa kuwa usajili ulikuwa haujafungwa, Kiongera aliondolewa kwenye orodha ya wachezaji wa Simba SC wa msimu uliopita ili nafasi yake asajiliwe mchezaji mwingine.
  Hata hivyo, Kiongera baada ya kupata nafuu alisajiliwa na KCB ambayo aliichezea katika Ligi Kuu ya Kenya.
  Baada ya kufunga mabao kadhaa ya kusisimua katika Ligi Kuu ya Kenya, Simba SC ilijiridhisha mshambuliaji huyo amepona na ikaamua kumrejesha kikosini.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIONGERA ATUA DAR KUJIUNGA NA SIMBA SC, DAKTARI ASEMA; “GOTI LAKE BADO BADO” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top