• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 27, 2015

  TIMU ZA AKINA BIN KLEB, BIG BON ZAANZA VYEMA KOMBE LA MWEZI MTUKUFU, ZATOA VICHAPO DIAMOND

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  TIMU mbili pacha, Chole United na Chole Rangers zimeanza vyema michuano ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa ushindi dhidi ya wapinzani wao, Milk Com na Water Com usiku huu Uwanja wa shule ya Diamond, Upanga, Dar es Salaam.
  Katika michuano hiyo ijulikanayo kama DFC 8 A Side Ramadhan, United walifungua dimba na Milk Com na kushinda 3-1, mabao yao yakifungwa na Abaly, Mudy Mass na Osama Muchacho.
  Rangers nao waliibuka na ushindi wa 1-0 bao pekee la Wera Wera na katika mchezo ujao wa Kundi A watacheza na DFC United wakati ndugu zao, United watacheza na DFC Rangers.


  Mmmoja wa wafadhili wa Chole zote, United na Rangers, Abdallah Ahmed Bin Kleb anayeshirikiana na Buye wa Big Bon amesema timu zao zote mbili zimejipanga kwa ajili ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
  “Tumejiandaa vyema na tunashukuru hatutumii mamluki, lakini vijana wa nyumbani kabisa wenye uwezo mkubwa ambao tunaamini mwisho wa siku watatupa ubingwa, wanafanya kazi nzuri” amesema Kleb.
  Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi kati ya DFC Rangers dhidi ya Sagger na DFC United dhidi ya Shibam Stars Uwanja huo huo wa Diamond, wakati Jumapili Young Legend dhidi ya Milk Com na DFC Makone dhidi ya Water Com, Jumatatu Milk Com watacheza DFC Rangers na Water Com DFC United. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIMU ZA AKINA BIN KLEB, BIG BON ZAANZA VYEMA KOMBE LA MWEZI MTUKUFU, ZATOA VICHAPO DIAMOND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top