• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 27, 2015

  ETOILE DU SAHEL YAANZA NA USHINDI MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

  TIMU ya Etoile du Sahel ya Tunisia imeanza kwa ushindi wa bao 1-0 hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stade Malien Uwanja wa Olympique de Sousse.
  Timu hiyo ya Tunisia iliyoitoa Yanga SC katika hatua ya 16 Bora, ilikutana na upinzani mkali kutoka kwa wageni wao, lakini ikadumu kuibuka na ushindi.
  Orlando Pirates ya Afrika Kusini nayo imeifunga AC Leopards bao 1-0 Uwanja wa Denis Sassou Nguesso mjini Dolisie, Kongo leo katika mchezo wa kwanza wa Kundi B Kombe la Shirikisho Afrika.
  Shukrani kwake, Happy Jele mfungaji wa bao hilo pekee la wababe hao wa Soweto wanaoanzia kileleni kwenye kampeni hizo.
  Pamoja na umati wa mashabiki wa wenyeji na hali mbaya ya Uwanja, lakini vijana wa Eric Tinkler walimudu kuondoka na ushindi ugenini.
  Mechi zijazo, The Beasts ya Niari itamenyana na CS Sfaxien wakati Pirates itaikaribisha Zamalek ya Misri Uwanja wa Mbombela Stadium mjini Nelspruit Julai 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ETOILE DU SAHEL YAANZA NA USHINDI MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top