• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 23, 2015

  MARIO MANDZUKIC ATUA JUVE MIAKA MINNE

  KLABU ya Juventus imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Croatia, Mario Mandzukic kutoka Atletico Madrid kwa ada ya Pauni Milioni 13.6.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekamilisha vipimo vya afya jana mjini Turin kabla ya kusaini Mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa Italia.
  Taarifa ya Juventus imesema: "Juventus inatangaza kwamba imefikia makubaliano na Atletico Madrid kwa usajili wa Maro Mandzukic kwa dau la Euro Milioni 19. 
  The 29-year-old striker completed a medical in Turin on Monday before putting pen to paper 
  Mario Maandzukic amefanhya vipimo vya afya jana mjini Turin kabla ya kusaini Mkataba wa miaka minne Juve

  Mandzukic anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa Juve kuelekea msimu mpya, baada ya awali kusajiliwa mshambuliaji wa Argentina, Paulo Dybala kutoka Palermo na Sami Khedira kutoka Real Madrid mapema mwezi huu.
  "NIna furaha kuwa katika klabu kubwa kama Juventus,' amesema Mandzukic na kuongeza; "Naamini kocha (Massimiliano Allegri) ananifahamu mimi vizuri sana na anajua anaweza kupata mazuri kutoka kwangu,"amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MARIO MANDZUKIC ATUA JUVE MIAKA MINNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top