• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 26, 2015

  YAMOTO BAND WAFUATA ‘LAMBO’ MAREKANI

  BENDI ya Yamoto inatarajiwa kwenda kutumbuiza nchini Marekani, Novemba mwaka huu, imeelezwa.
  Mmiliki wa yamoto Band, wanaotamba kwa sasa nchini, Said ‘Mkubwa’ Fela ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba tayari wamepata mwaliko huo na kwa sasa wapo katika matayarisho ya ziara hiyo.
  Fela amesema kwamba hayo ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na bendi yake kwa sasa nchini na wanajipanga vizuri kwenda kufanya mambo ya kihistoria Marekani.
  “Siku zote kazi ngumu inalipa. Nasi tunajivunia jasho letu kwa sasa, zipo ziara nyingi tu za nje zinakuja na tuna mialiko mingi kutoka nchi mbalimbali duniani, wakati ukifika wananchi watajua,”amesema Fela.
  Kwa sasa kundi hilo lipo katika mapumziko ya kuupisha mwezi mtukufu wa Ramadhani na abaada ya mfungo huo, itaendelea na maonyesho yake kama kawaida nchini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YAMOTO BAND WAFUATA ‘LAMBO’ MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top