• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 28, 2015

  BRAZIL YATUPWA NJE COPA AMERICA, PARAGUAY WASONGA KWA MATUTA

  BRAZIL imetupwa nje ya michuano ya Copa America baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 na Paraguay kufuatia sare ya 1-1 katika Robo Fainali usiku huu Uwanja wa Ester Roa Rebolledo nchini Chile.
  Mkongwe Robinho alianza kuifungia Brazil dakika ya 15, kabla ya Derlis Gonzalez kuisawazishia Paraguay kwa penalti dakika ya 70.
  Kikosi cha Ramon Diaz kikaenda Nusu Fainali kwa mara ya pili mfululizo kwa ushindi wa penalti 4-3.
  Penalti za Paraguay zilifungwa na Martinez, V Caceres, Bobadilla na Gonzalez wakati Santa Cruz alikosa na kwa upande wa Brazil, waliofunga ni Fernandinho, Miranda na Coutinho, huku Ribeiro na Douglas Costa wakikosa.
  Kikosi cha Paraguay kilikuwa; Villar, Aguilar, Da Silva, B Valdez, Piris, Gonzalez, V Caceres, Aranda/Martinez, Benitez/Romero dk84, Santa Cruz na N Valdez/Bobadilla dk73.
  Brazil; Jefferson, Alves, Silva, Miranda, Filipe Luis, Fernandinho, Elias, Willian/Costa dk60 Coutinho, Robinho/Ribiero dk87, Firminho/Tardelli dk69.
  Brazil players look dejected after the defeat to Paraguay on penalties in the quarter-finals in Concepcion
  Wachezaji wa Brazil wakiwa na masikitiko baada ya kutolewa kwa penalti na Paraguay katika Robo Fainali ya Copa America PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BRAZIL YATUPWA NJE COPA AMERICA, PARAGUAY WASONGA KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top